ZIARA YA MHE. RAIS WA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI DKT. HUSSEIN ALI MWINYI, TUMBE WILAYA YA MICHEWENI PEMBA

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi ameeleza kuna umuhimu mkubwa kwa familia zitakazokabidhiwa nyumba, kituo cha afya, shule, msikiti pamoja na maduka kuvitumia ipasavyo kwa kuhakikisha wanavitunza ili visipoteze haiba yake.

Rais Dkt. Mwinyi aliyasema hayo Ijumaa tarehe 12/03/2021 huko Tumbe Wilaya ya Micheweni Kisiwani Pemba wakati alipotembelea Mradi wa Kijiji cha Makaazi ya Wananchi walioathiriwa na mvua za masika za mwaka 2017, uliojengwa kwa ufadhili wa Emirates Red Crescent.

Mapema,  alipatiwa maelezo kuhusu mradi huo na Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa pili wa Rais, Sera, Uratibu na Baraza la Wawakilishi Ndg. Thabit Idarous Faina wakati alipotembelea maeneo tofauti ya mradi huo.

*KITENGO CHA UHUSIANO
KAMISHENI YA KUKABILIANA NA MAAFA ZANZIBAR.*