MAKAMU WA PILI WA RAIS WA ZANZIBAR MHE. HEMED SULEIMAN ABDULLA AKIWAELEZA WAWEKEZAJI WA KAMPUNI YA SOFTLINE KUTOKA NCHINI URUSI

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar  Mhe. Hemed Suleiman Abdulla amesema serikali ya mapinduzi Zanzibar imefungua milango yake kwa waekezaji wa sekta binafsi kutoka ndani na nje ya nchi kuekeza katika miradi mbali mbali kwa lengo la kuinua uchumi wa nchi na kuimarisha ustawi wa wananchi wake.

Mhe. Hemed alilieza hayo wakati akizungumza na viongozi na wataalamu wa Kampuni ya SoftLine kutoka nchini Urusi waliofika ofisini kwake Vuga jijini Zanzibar kwa lengo la kuwasilisha mpango wao na kuonesha nia ya kuekeza kupitia mradi wa mji Salama.

Aliwaeleza viongozi hao kuwa, serikali ya Mapinduzi Zanzibar imefungua milango yake kwa kuwakaribisha wawekezaji kuja kuekeza kupitia sekta mbali mbali ikiwemo miundo mbinu ya barabara, Umeme,sekta ya viwanda, pamoja na sekta ya uvuvi ili kuinua uchumi wa Zanzibar kama serikali ilivyopambanua juu ya adhma yake hiyo.

Akigusia juu ya mradi wa mji salama ambao kampuni hiyo imeonesha nia yake ya kuekeza Makamu wa Pili wa Rais aliwaeleza wawekezaji hao kwamba, kwa vile Zanzibar ni nchi kisiwa kama zilivyo nje nyengine akitolea mfani nchi ya Moritus alisema inahitaji miradi ya aina hiyo kwa lengo la kuimarisha usalama wa watalii wanaofika nchini.

Mhe. Hemedi alisema kwa vile Zanzibar inategemea sekta ya utaali kwa kiasi kikubwa hivyo, kuna haja ya kuimarisha mazingira ya usalama kwa wageni wanaofika nchini sambamba na kuhakisha usalama wa mji na maeneo yake yote.

“Niseme tu Zanzibar inahitaji sana mradi wa kuimarisha mji salama kwa usalama wa  wataalii wanaofika Zanzibar” Alieleza Mhe. Hemed

Makamu wa Pili wa Rais alitumia fursa hiyo kuwaelekeza wawekezaji hao kuandaa andiko lao la mradi na kuliwasilisha serikalini kupitia wizara husika inayohusiana na masuala ya uwekezaji ili kufuata taratibu na mingozo inavyoelekeza.

Aliwahakikishia wawekezaji hao kuwa serikali ya awamu ya nane inayoongozwa na Rais Dk. Hussein Ali Mwinyi imeweka mazingira mazuri ya waekezaji wanaotaka kuekeza Zanzibar kwa kuweka kipindi kifupi cha kupata majibu kwa muekezaji yoyote anaetaka kuekeza Zanzibar ikiwa lengo ni kuondoa urasimu na usumbufu kwa wawekezaji wake.

“Napenda kuwahakikishia serikali yetu haina urasimu kwa wawekezaji walionesha nia ya kuekeza nchini kwetu, jambo la msingi naomba mufuate sharia na taratibu za nchu yetu zinavyolekeza” Alisisitiza Makamu wa Pili.

Mhe. Hemed alisema serikali inaendelea kuimarisha mazingira mazuri ya uwekezaji kwa kuzipitia na kuzifanyia marekebisho sheria mbali mbali ili ziweze kutoa urahsi Zaidi kwa wawekezaji kwa kuzingatia upatikanaji wa maslahi baina ya pande mbili (Win Win Situation)

Kwa upande wake Mkurugenzi wa maendeleo ya bishara kutoka kampuni ya Softline Evgeniy Chizhov alimueleza Mhe. Makamu wa Pili wa Rais kuwa kampuni yao ina uzoefu mkubwa katika masuala ya kuimarisha ulinzi wa miji kutokana na kufanya kazi kwake kwa muda mrefu sasa.

Alisema Kampuni yao imekuwa ikitekeleza miradi yake kupitia nchi tofati na imezaa matunda kwa kufanikiwa kuzuwia matukio ya kihalifu sambamba na kuweka udhibiti mzuri juu ya matumizi ya sheria na kanuni za barabarani.

Wakiwasilisha mpango wa kampuni yao wataalamu kutoka kampuni ya Softline kutoka nchini Urusi Bw. Vitaliy Razzhvin na Bibi Alla Bochkreva walisema kampuni yao pamoja na umarishaji wa Miji lakini pia wana uwezo wa kufunga mitambo itakayosaidia kuzuwia uhalifu unaotendeka kwa njia ya baharini akitolea mfano uwezo wa kuzuwia tatizo la uvuvi haramu.

Kampuni ya Softline kutoka Urusi imeshatekeleza miradi na kufanya kazi zake katika nchi mbali mbali ikiwemo India, Bangladeshi na Nchi nyengine mbali mbali zilizopo katika muunganiko wa iliokuwa muungano wa nchi za Sovieti.

……………………………………..

Kassim  Abdi

Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais

Zanzibar.