![]() |
ZANZIBAR DISASTER MANAGEMENT COMMISSION |
![]() |
---|
SIKU YA KUZUIWA KUZAMA DUNIANI |
---|
![]() |
Dunia ikiwa inaelekea katika kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Kuzuia Kuzama Duniani (Drowning Prevention Day) tarehe 25 Julai ya kila mwaka.
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Kamisheni ya Kukabiliana na Maafa itaadhimisha siku hiyo mnamo tarehe 28 Julai 2025 katika maeneo ya Forodhani nyuma ya Hotel ya Tembo Hotel majira ya saa nane (8:00) mchana hivyo, inawaalika wadau wote zikiwemo taasisi za Serikali na binafsi, wavuvi, wakulima wa mwani, wapiga makachu, wamiliki wa vyombo vya usafiri na mwananchi mmoja mmoja. Miongoni mwa shughuli zitakazofanyika siku hiyo ni pamoja na:-
Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo anatarajiwa kuwa Mheshimiwa Hamza Hassan Juma Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Kauli Mbiu ya Maadhimisho ya mwaka huu ‘Hadithi yako inaweza kuokoa maisha’ |