ZANZIBAR DISASTER MANAGEMENT COMMISSION |
---|
KUGHAIRISHWA KWA SHUGHULI YA UZINDUZI WA VIJIJI VYA MAKAAZI YA WANANCHI WALIOATHIRIWA NA MVUA ZA MASIKA ZA MWAKA 2017, NUNGWI. |
---|
TAARIFA KWA UMMA
AFISI YA MAKAMU WA PILI WA RAIS, SERA, URATIBU NA BARAZA LA WAWAKILISHI INAWATANGAZIA VIONGOZI NA WANANCHI WOTE KUWA ILE SHUGHULI YA UZINDUZI WA VIJIJI VYA WANANCHI WALIOATHIRIWA NA MVUA ZA MASIKA ZA MWAKA 2017 ILIOTARAJIWA KUFANYIKA TAREHE 06 NOVEMBA 2021 NUNGWI KASKAZINI A UNGUJA, IMEGHAIRISHWA. HII NI KUTOKANA NA SABABU ZISIZOWEZA KUEPUKIKA.
AFISI INAOMBA RADHI KWA WAALIKWA NA WANANCHI WOTE KWA USUMBUFU WOWOTE UTAKAOJITOKEZA. AIDHA, TAARIFA NYENGINE KUHUSIANA NA SHUGHULI HIYO ITATOLEWA HAPO BAADAE.
IMETOLEWA NA: AFISI YA MAKAMU WA PILI WA RAIS (SERA, URATIBU NA BARAZA LA WAWAKILISHI) 03, NOVEMBER 2021.
|