JITIHADA MBALIMBALI ZAFANYIKA KUTOKOMEZA KIPINDUPINDU ZANZIBAR

Katika kutekeleza azma ya Serikali ya kutokomeza Kipindupindu Zanzibar, Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Sera, Uratibu na Baraza la Wawakilishi  Ndugu Thabit Idarous Faina ameongoza kikao cha Kamati ya Uongozi ya kusimamia utekelezaji wa mpango wa kutokomeza kipindupindu Zanzibar( ZACCEP) mapema leo tarehe 03 Septemba, 2021 kilichofanyika katika ukumbi wa Tume ya Uchaguzi (ZEC) Maisara Zanzibar.

 

Mpango huu una lengo la kutokomeza kabisa kipindupindu Zanzibar ndani ya miaka 10 hadi kufikia mwaka 2018.

 

Uwepo wa Kikao hichi kimekuja kutokana na matakwa ya kufanyika kwake kwa kila mwaka kwa lengo la kutathmini utekelezaji wa mpango huu ili kuweza kubaini mafanikio pamoja na changamoto zilizopo ili kuweza kuzitaftia ufumbuzi.

 

Miongoni mwa hatua zilichokuliwa katika utekelezaji wa mpango huu ni pamoja na Usambazaji wa Maji safi na salama kazi inayofanywa na taasisi ya Mamlaka ya maji Zanzibar (ZAWA) pamoja na kupatiwa chanjo wananchi ya kuzuia kipindupindu ilioanza kutolewa hivi karibuni kupitia Wizara ya Afya, Ustawi wa jamii, Wazee, Jinsia na Watoto.

 

Pamoja na mambo mengine, kikao hichi kilipokea taarifa ya kazi ya Ufuatiliaji na Tathmini ya Utekelezaji wa Mpango wa kutokomeza kipindupindu Zanzibar kuanzia 2018-2021.

 

Picha na Abubakar Mussa Ibrahim,
Kamisheni ya Kukabiliana na Maafa Zanzibar